WFN Naturals

Weka oda

Mchakato

Jinsi ya kuagiza bidhaa

Bofya mara moja kwenye simu yako ya kiganjani ujipatie bidhaa muhimu uipendayo kwa kuweka oda kupitia tovuti ya WFN Naturals na utafikishiwa bidhaa yako mahali ulipo kwa haraka na kwa uaminifu mkubwa. Ni rahisi kununua bidhaa mtandaoni kupitia kwenye tovuti ya WFN Naturals ( inapofunguka ), kwa kufuata hatua kadhaa zifuatazo

Hatua 1

Chagua bidhaa unayohitaji kununua kisha, nenda kwenye ukurasa wa bidhaa kwa kubofya kitufe cha menyu, halafu chagua kichupo (tab) cha bidhaa (products). Ukibonyeza kichupo cha bidhaa, utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa bidhaa. Bofya kwenye bidhaa unayohitaji kununua kisha chagua kiasi unachohitaji kununua na bonyeza weka kwenye kikapu.

Hatua 2

Fanya marejeo ya oda yako kwa kubofya, tazama kikapu chako (view basket) ili kujiridhisha na bidhaa uliyoichagua, kiasi, pamoja na bei itakayojumuisha pia gharama za usafirishaji wa mzigo wako mpaka kwenye eneo la makazi yako. Ikiwa umeridhika na uchaguzi wako, unaweza kuendelea na hatua inayofuata kwa kubofya endelea kutoka (proceed to checkout). Ili kuongeza bidhaa nyingine zaidi utahitaji kurejea tena kwenye ukurasa wa bidhaa na uirudie tena hatua hii kwenye bidhaa lengwa.

Hatua 3

Jaza taarifa zinazohitajika kwenye fomu inayoonekana kisha chagua njia ya malipo. Malipo ya WFN Naturals yanaweza kufanyika kwa namna nyingi; Kama utachagua kulipa moja kwa moja ya basi lipa kupitia njia ya malipo inayojitokeza kwenye ukurasa wa kutoka (checkout page) na oda yako itashughulikiwa na kusafirishwa kwako pale malipo yako yalipothibitishwa. Tumia namba ya oda yako (WFNXXXX) kama rejea unapofanya malipo. Vile vile unaweza kuchagua kulipia penye duara la malipo ya Pesa pal ambayo inakuruhusu kufanya malipo kupitia huduma za malipo za mitandao ya simu au kadi za malipo. Pale malipo yanapokamilika, tutaishughulikia oda yako na kuituma haraka iwezekanavyo.

Q&A

Maswali na majibu

Ikiwa jedwali hili hapa chini haliwezi kutoa jibu sahihi la swali lako, tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano na tutakupatia ufumbuzi kwa haraka zaidi

1. Itachukua muda gani kuweza kupokea oda yangu?

Itakuchukua muda wa dakika 30-60 kama upo Dar es Salaam, Pwani, Singida na Ifakara na saa 6-24 kwa mikoa ya Morogoro, Iringa na Tanga kupokea oda yako tangu muamala wako ulipothibitishwa. Kwa mikoa mingine ya Tanzania ni saa 12-24 utapata mzigo wako tangu malipo ya oda yako yalipothibitishwa.

Kwa wateja wengine wa Afrika ya Mashariki(Nairobi, Mombasa, Kampala,Kigali, Bujumbura) itakuchukua siku mbili mpaka siku tatu mzigo kukufikia katika ofisi za wasafirishaji kwenye miji husika tayari kwa kuchukuliwa. Mteja atapigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno kuwa mzigo wake umefika na anapaswa kwenda kuupokea.

Kwa wateja wa DRC (Lubumbashi, Goma, Bukavu, Uvira) itakuchukua siku nne mpaka tano mzigo kumfikia mteja wetu.

2. Je, ni salama kuweka oda kwenye tovuti yenu?

Malipo yote yanayoshughulikiwa na Pesa pal na yanalindwa na Verisign SSL. Kutazama sera yetu ya faragha tafadhali bonyeza hapa.

3. Ninatumiaje kuponi kwenye tovuti ya WFN Naturals?

Tumekuwa na utaratibu wa kuwapa punguzo wateja wetu kwa njia ya kuponi ambayo inawaruhusu kupata bidhaa fulani kwa punguzo maalumu la bei. Ni rahisi, kopi na kisha pachika/andika kuponi yako kwenye sehemu ya visanduku vya kujaza namba za kuponi kwenye kikapu/ukurasa wa kutoka na kisha omba kuponi yako. Punguzo lako litaratibiwa moja kwa moja.

4. Nitafanyaje ikiwa nimepata shida yoyote juu ya oda yangu?

Tuma barua pepe kupitia info@wfn.co.tz na kisha mshauri kutoka timu ya WFN Naturals atakuitikia na kukupatia huduma juu ya maulizo yako.

5. Naweza kuweka oda kisha nije kuichukua mwenyewe?

Hapana. Kwa sasa manunuzi ya mtandaoni na manunuzi ya ana kwa ana yanashughulikiwa kwa utofauti.